Naamini
wote tunajua umuhimu wa wakalimani wa lugha ya alama kurahisisha mawasiliano
katika shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo ni muhimu kwa watu wenye
uziwi.Wakalimani ni viungo muhimu sana kwa
jamii ya viziwi ulimwenguni kote,Sote tushawahi kuona umahiri wa wakalimani
kwenye taarifa za habari pale anapofasiri kwa umaridadi wa lugha ya alama ili
viziwi waweze kuelewa kile kinachozungumzwa na wahusika vile vile hata shuleni wakalimani wana umuhimu katika kuwafanya
viziwi waweze kuelewa kile ambacho mwalimu anakifundisha siyo hivyo tu hata
mahakmani pia wakalimani wanahitajika.
Katika
nchi za wenzetu walioendelea suala la ukalimani wa lugha ya alama siyo tatizo
sana kama katika nchi zetu za Afrika hususani Tanzania.Nchi kama Finland ambayo
inasifika kutoa elimu nzuri kwa watu
wenye ulemavu. Suala la ukalimani kwao
limepewa kipaumbele sana ili kuwasahidia viziwi kufanikisha shughuli zao ndiyo
maana angalau kila kiziwi anapata mkalimani mmoja kwa matumizi yake na serikali yao inawajibika kuwalipia
huduma waliyopata kutoka kwa mkalimani.
Wakati
huku kwetu Tanzania suala la ukalimani ni mwiba mchungu unaosababisha maumivu makali kwa viziwi kila siku.Mwiba huo
unawachoma kote kote.Wakalimani walio wengi hapa Tanzania hawana mafunzo ya
mbinu bora za ukalimani,maadili ya ukalimani,kutokuheshimu siri za wateja wao
ambao ni viziwi na kutokuheshimu mipaka ya kazi.Ila wachache waliopo
wanajitahidi kufuata hizo kanuni chache kwa ufasaha.
Siku
zote mkalimani ni mtoa huduma kwa viziwi na viziwi ni wapokea huduma kwa dhana hiyo kiziwi ana haki ya kutoa malalamiko kama
huduma anayopata kutoka kwa mkalimani ni mbaya na haijamridhisha kwaiyo anaweza
kuchukua hatua yoyote anayoona inafaa kwake kama vile kumuondoa kwa kufuata
taratibu na sheri walizowekeana na kufanya mchakato wa kumtafuta mkalimani mpya ambaye anahisi
atamuelewa vizuri.Hivyo mkalimani atabaki tu kuwa mtoa huduma ya kufasiri
mawasiliano kati ya mteja wake ambaye ni kiziwi na mtu yoyote mwenye shida na
kiziwi.Hapa mkalimani anapaswa kufikisha ujumbe sahihi kwa mteja wake kwa maana
ya huduma bora pia anapaswa kutokuongeza maneno au kutoka nje ya mada kwa maana
nyingine kwamba aheshimu mazungumzo ya mteja wake na kutomuingilia mteja wake.
Maendeleo
ya sayansi na teknolojia yameleta mafanikio mengi siku hizi viziwi hawatumii barua kuwasiliana
na wenzi wao au marafiki zao kwa kutumia
teknolojia ya video inayowawezesha kuonana wao kwa wao ambayo inapatikana
katika mitandao ya kijamii licha ya mafanikio hayo kuna changamoto nyingi sana
changamoto hizo naweza kuzifananisha na wakalimani
wa lugha ya alama tishio la ajira kwa viziwi.
Kumezuka
wimbi kubwa la wakalimani wasio
waaminifu na wasio fuata maadili ya ukalimani wao kwa kutumia uelewa wao mdogo
au mkubwa hujifanya wao ndio wasemaji
wakuu wa viziwi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo jambo ambalo si
sahihi bali makalimani yoyote yule mwenye maadili ya ukalimani anajua miiko na mipaka ya ukalimani kama tafsiri ya neno ukalimani wa lugha ya alama linavyoeleza .Kiziwi atabaki kuwa msemaji mkuu wa mambo yote
yanayomuhusu yeye na jamii yake ila mkalimani atafasiri yale yote ambayo kiziwi
ameyazungumza kwa kutumia lugha ya alama.
Kuna
watu wengi wanajifanya wao ni wakalimani
wa viziwi na kuipotosha jamii ya Tanzania kwa kuwaeleza tamaduni za viziwi kitu
kinachotia mashaka kwamba hakuna uhalisia wowote kuhusu wanachoongelea kwani
wanakua hawana uzoefu nao ila mtu sahihi wa kuulizwa hapa ni kiziwi mwenyewe.
Kutokana
na tafsiri ya ukalimani wa lugha ya alama haielezi kwamba atakuja kuwa mwalimu
wa lugha ya alama bali inasema atakua mkalimani wa lugha ya alama.Ila
wakalimani walio wengi wanaacha shughuli zao za ukalimani na kuingilia shughuli
za kufundisha lugha ya alama kitu kinachochangia ukosefu wa ajira kwa viziwi na
hata kuipotosha jamii kuhusu uhalisia wa viziwi kwa ujumla ni vizuri mkalimani
akaheshimu kazi yake na mipakayake siyo kuruka ruka kila sehemu.
Athari
si ukosefu wa ajira tu ila zipo nyingi kwamba jamii kuendelea kuwaona viziwi ni
kundi lisilojiweza yaani haliwezi kufanya kazi yoyote,Jamii haitaweza
kubadilika kwa sababu mkalimani anapogeuka kuwa msemaji wa viziwi jamii
itamuona ni mtu wa kawaida sawa na wao, watu wengi wanapenda mifano halisi
kutoka kwa wahusika wenyewe ili wajifunze kitu halisi ndiyo maana wenzetu
katika nchi zilizoendelea wanawatumia wahusika wenyewe pia kukosekana uhalisia
wa kile kinachofundishwa na mkalimani.
Jamii
itawaona na kuamini kwamba viziwi wenyewe wanaweza kufanya kazi yoyote hata ya
kiofisi pale wanapofanya kazi wenyewe hii itasaidia kuondokana na imani potofu
kwamba viziwi kazi zao ni za kutumia nguvu kama vile ufundi ujenzi na kadhalika
na kazi zinazohitaji kutumia akili ni kazi za kuwakilishwa.
Kama
wewe ni mkalimani unayejitambua fuata
maadili ya ukalimiani pia heshimu mipaka ya kazi yako kutokanana na tafsiri ya
neno ukalimani wa lugha ya alama.
Kahaya
0719999861
Whatsapp
Maneno kuntu kamanda ila sijui kama yamefika masafa marefu. 😁😁😁😁
JibuFutaMaana Sijaona wachangiaji hapa
Kikubwa tu ni kwamba kweli wapo wakalimani ambao wanapotosha ukweli wanaufanya uonga muda mwingi huwapondea viziwi wao. Ila ninachoona muda mwingine viziwi wanaoelewa lugh ya alama fasihi wapo wachache sana Tanzania hivyo ni sahihi walimu na wakalimani kusaidia ufundishaji wa lugha ya kwa wahitaji ili lugha hii iweze kuenea kwa haraka na kwa urahisi
JibuFutaUkalimani wa lugha ya alama Ni taaluma Kama zilivyo taaluma nyingine Kama vile ualimu, wanasheria na utangazaji. Moja ya sifa kuu ya taaluma yoyote duniani ni kuwa na umoja pamoja mfumo wa maadili (association & ethical foundation). Kinachopelekea kuwepo kwa hao wakalimani wa lugha ya alama matapeli naweza kusema, Ni kukosekana kwa sheria na sera madhubuti zinazotuunganisha/zinatuelekeza wakalimani wote juu ya misingi ya ukalimani. Kupitia umoja wa wakalimani wa lugha tunaweza kuwa tunakumbushana juu ya misingi hiyo na kuwachukulia sheria wale wote wanaokiuka.
JibuFutaMpaka hapo itoshe kusema kwamba Ni myda sasa wa wadau (deaf community),selikari pamoja na mashirika binafsi kuunganisha nguvu na kutengeneza sera madhubuti juu ya msitakhbari wa viziwi Katika jamii. Ahsante!