Jumatatu, 13 Novemba 2017

WAKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA TISHIO LA AJIRA KWA VIZIWI

Naamini wote tunajua umuhimu wa wakalimani wa lugha ya alama kurahisisha mawasiliano katika shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo ni muhimu kwa watu wenye uziwi.Wakalimani  ni viungo muhimu sana kwa jamii ya viziwi ulimwenguni kote,Sote tushawahi kuona umahiri wa wakalimani kwenye taarifa za habari pale anapofasiri kwa umaridadi wa lugha ya alama ili viziwi waweze kuelewa kile kinachozungumzwa na wahusika vile vile hata shuleni  wakalimani wana umuhimu katika kuwafanya viziwi waweze kuelewa kile ambacho mwalimu anakifundisha siyo hivyo tu hata mahakmani pia wakalimani wanahitajika.

Katika nchi za wenzetu walioendelea suala la ukalimani wa lugha ya alama siyo tatizo sana kama katika nchi zetu za Afrika hususani Tanzania.Nchi kama Finland ambayo inasifika  kutoa elimu nzuri kwa watu wenye  ulemavu. Suala la ukalimani kwao limepewa kipaumbele sana ili kuwasahidia viziwi kufanikisha shughuli zao ndiyo maana angalau kila kiziwi anapata mkalimani mmoja  kwa matumizi yake na serikali yao inawajibika kuwalipia huduma waliyopata kutoka kwa mkalimani.
Wakati huku kwetu Tanzania suala la ukalimani ni mwiba mchungu unaosababisha maumivu  makali kwa viziwi kila siku.Mwiba huo unawachoma kote kote.Wakalimani walio wengi hapa Tanzania hawana mafunzo ya mbinu bora za ukalimani,maadili ya ukalimani,kutokuheshimu siri za wateja wao ambao ni viziwi na kutokuheshimu mipaka ya kazi.Ila wachache waliopo wanajitahidi kufuata hizo kanuni chache kwa ufasaha.

Siku zote mkalimani ni mtoa huduma kwa viziwi na viziwi ni wapokea huduma kwa dhana  hiyo kiziwi ana haki ya kutoa malalamiko kama huduma anayopata kutoka kwa mkalimani ni mbaya na haijamridhisha kwaiyo anaweza kuchukua hatua yoyote anayoona inafaa kwake kama vile kumuondoa kwa kufuata taratibu na sheri walizowekeana na kufanya mchakato wa  kumtafuta mkalimani mpya ambaye anahisi atamuelewa vizuri.Hivyo mkalimani atabaki tu kuwa mtoa huduma ya kufasiri mawasiliano kati ya mteja wake ambaye ni kiziwi na mtu yoyote mwenye shida na kiziwi.Hapa mkalimani anapaswa kufikisha ujumbe sahihi kwa mteja wake kwa maana ya huduma bora pia anapaswa kutokuongeza maneno au kutoka nje ya mada kwa maana nyingine kwamba aheshimu mazungumzo ya mteja wake na kutomuingilia mteja wake.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta mafanikio mengi  siku hizi viziwi hawatumii barua kuwasiliana na wenzi wao au marafiki zao  kwa kutumia teknolojia ya video inayowawezesha kuonana wao kwa wao ambayo inapatikana katika mitandao ya kijamii licha ya mafanikio hayo kuna changamoto nyingi sana changamoto hizo naweza kuzifananisha na wakalimani wa lugha ya alama tishio la ajira kwa viziwi.

Kumezuka  wimbi kubwa la wakalimani wasio waaminifu na wasio fuata maadili ya ukalimani wao kwa kutumia uelewa wao mdogo au mkubwa  hujifanya wao ndio wasemaji wakuu wa viziwi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo jambo ambalo si sahihi bali makalimani yoyote yule mwenye maadili ya ukalimani anajua miiko na  mipaka ya ukalimani kama tafsiri ya neno ukalimani wa lugha ya alama linavyoeleza .Kiziwi  atabaki kuwa msemaji mkuu wa mambo yote yanayomuhusu yeye na jamii yake ila mkalimani atafasiri yale yote ambayo kiziwi ameyazungumza kwa kutumia lugha ya alama.

Kuna watu wengi  wanajifanya wao ni wakalimani wa viziwi na kuipotosha jamii ya Tanzania kwa kuwaeleza tamaduni za viziwi kitu kinachotia mashaka kwamba hakuna uhalisia wowote kuhusu wanachoongelea kwani wanakua hawana uzoefu nao ila mtu sahihi wa kuulizwa hapa ni kiziwi mwenyewe.

Kutokana na tafsiri ya ukalimani wa lugha ya alama haielezi kwamba atakuja kuwa mwalimu wa lugha ya alama bali inasema atakua mkalimani wa lugha ya alama.Ila wakalimani walio wengi wanaacha shughuli zao za ukalimani na kuingilia shughuli za kufundisha lugha ya alama kitu kinachochangia ukosefu wa ajira kwa viziwi na hata kuipotosha jamii kuhusu uhalisia wa viziwi kwa ujumla ni vizuri mkalimani akaheshimu kazi yake na mipakayake siyo kuruka ruka kila sehemu.
Athari si ukosefu wa ajira tu ila zipo nyingi kwamba jamii kuendelea kuwaona viziwi ni kundi lisilojiweza yaani haliwezi kufanya kazi yoyote,Jamii haitaweza kubadilika kwa sababu mkalimani anapogeuka kuwa msemaji wa viziwi jamii itamuona ni mtu wa kawaida sawa na wao, watu wengi wanapenda mifano halisi kutoka kwa wahusika wenyewe ili wajifunze kitu halisi ndiyo maana wenzetu katika nchi zilizoendelea wanawatumia wahusika wenyewe pia kukosekana uhalisia wa kile kinachofundishwa na mkalimani.

Jamii itawaona na kuamini kwamba viziwi wenyewe wanaweza kufanya kazi yoyote hata ya kiofisi pale wanapofanya kazi wenyewe hii itasaidia kuondokana na imani potofu kwamba viziwi kazi zao ni za kutumia nguvu kama vile ufundi ujenzi na kadhalika na kazi zinazohitaji kutumia akili ni kazi za kuwakilishwa.
Kama wewe ni mkalimani  unayejitambua fuata maadili ya ukalimiani pia heshimu mipaka ya kazi yako kutokanana na tafsiri ya neno ukalimani wa lugha ya alama.

Kahaya
0719999861

Whatsapp

Maoni 3 :

  1. Maneno kuntu kamanda ila sijui kama yamefika masafa marefu. 😁😁😁😁
    Maana Sijaona wachangiaji hapa

    JibuFuta
  2. Kikubwa tu ni kwamba kweli wapo wakalimani ambao wanapotosha ukweli wanaufanya uonga muda mwingi huwapondea viziwi wao. Ila ninachoona muda mwingine viziwi wanaoelewa lugh ya alama fasihi wapo wachache sana Tanzania hivyo ni sahihi walimu na wakalimani kusaidia ufundishaji wa lugha ya kwa wahitaji ili lugha hii iweze kuenea kwa haraka na kwa urahisi

    JibuFuta
  3. Ukalimani wa lugha ya alama Ni taaluma Kama zilivyo taaluma nyingine Kama vile ualimu, wanasheria na utangazaji. Moja ya sifa kuu ya taaluma yoyote duniani ni kuwa na umoja pamoja mfumo wa maadili (association & ethical foundation). Kinachopelekea kuwepo kwa hao wakalimani wa lugha ya alama matapeli naweza kusema, Ni kukosekana kwa sheria na sera madhubuti zinazotuunganisha/zinatuelekeza wakalimani wote juu ya misingi ya ukalimani. Kupitia umoja wa wakalimani wa lugha tunaweza kuwa tunakumbushana juu ya misingi hiyo na kuwachukulia sheria wale wote wanaokiuka.
    Mpaka hapo itoshe kusema kwamba Ni myda sasa wa wadau (deaf community),selikari pamoja na mashirika binafsi kuunganisha nguvu na kutengeneza sera madhubuti juu ya msitakhbari wa viziwi Katika jamii. Ahsante!

    JibuFuta