Ulemavu ni hali inayowakabili watu wengi duniani na hali inaweza kusababishwa na mambo mengi sana kama vile ajali,matumizi mabaya au kupindukia ya dawa na madawa ya ya kulevya kwa mama mjamzito.ulemavu umegawanyika katika makundi mbalimbali kama vile wasioona,Viziwi,Albino,walemavu wa mtindio wa ubongo,walemavu wa viungo,viziwi wasioona.kila kundi hapo linakabiliwa na changamoto zake katika jamii hususani walemavu wa viungo kama tunavyoona pichani hapo wanakabiliwa na miundombinu isiyo rafiki kwao hakuna majengo yanayowawezesha walemavu wa viungo kuweza kupita bila shida.Ninapooangalia picha hii najiuliza kweli tutafika???licha ya jamii kutunyanyampaa sababu ya utegemezi wetu lakini miundombinu nayo siyo rafiki kwetu.Uongozi wa JPM unapaswa kuliangalia hili suala kwa jicho la tatu kama kweli wamezamilia kweli watu wenye ulemavu waondokane na utegemezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni