Watu wengi wanashindwa
kuwasiliana na watoto viziwi kwa kufikiri kwamba lazima awepo mkalimani wa
lugha ya alama au Mwalimu wa viziwi ndiyo watu pekee wa kuweza kuwasiliana nao
jambo ambalo siyo sahihi.Mambo yafuatayo ukiyazingatia kwa ukamilifu
yatakusaidai kuweza kuwasiliana na watoto viziwi;
1. Hakikisha
kwamba unateka makini ya mtoto kabla hujaanza kuongea naye.Jaribu kumpungia
mkono au kumgusa kidogo begani.(usimrushie jiwe,usimwite kwa kumpigia makofi)
2. Mtizame
yule mtoto ana kwa ana unapoongea naye.Kila mara hakikisha kuwa mtoto huyo
anaweza kuuona uso wako vyema.Ikibidi keti au chuchumaa ili uso wake uwe
sambamba na wako.
3. Tumia
vitu vinavyoonekana iwezekanavyo.Ashiria kwa mkono kitu au kifaa
unachozungumzia.
4. Mweleze
mtoto mada unayozungumza au mjulishe unapobadilisha mada.
5. Simama
uso wako ukitizama kwenye mwangaza.
6. Jaribu
kumwambia arudie kile au yale uliyoyasema iwapo huna hakika kama amekuelewa.
7. Mra
nyingi mazungumzo ya vikundi yanaweza kuwa magumu kwa mtoto kiziwi.Mshirikishe
kila hatua.Hakikisha kuwa wanazungumza kwa zamu.
Upo sahihi kijana
JibuFutaAsante kwa uelimishaji tutazingatia yote ili tuweze kufanikisha malengo waliyinayo watoto Hawa wenye mahitaji maalum
JibuFuta